Kitu chochote unachokilalamikia au kulaumu kwenye maisha yako, unakistahili kabisa. Na kadiri utakavyoendelea na malalamiko na lawama zako, utaendelea kuwa na kitu hicho.
Hakuna namna mambo yataenda kama unavyopanga wewe, hivyo kulalamikia watu au hali fulani kuwa kikwazo kwako ni utoto. Na kama hujui hilo, basi unastahili kabisa kile kilichokutokea.
Kama unamlalamikia mtu ambaye ulimwamini na akakuangusha, basi jua unastahili kabisa kuangushwa. Kwa sababu ulipuuza ukweli kwamba watu huwa wanafanya mambo ambayo hatuwategemei kufanya, hivyo pamoja na kuwaamini, ni muhimu kuwa na tahadhari. Kama ulifikiri huyo ni wa tofauti na ukamwamini bila tahadhari, basi unastahili alichokufanyia na kama hutajifunza utaendelea kukutana na hali kama hiyo.
Kama unamlalamikia mwajiri wako kwamba hakulipi vizuri au hajali kazi unayofanya, unastahili kabisa hicho anachokufanyia. Mwajiri wako atakuwa anakufanyia hivyo kwa sababu haogopi kukupoteza, anajua hata ukiondoka hakuna anachokosa. Kama ungekuwa unafanya vitu vya tofauti, ambavyo wengine hawawezi kufanya, lazima mwajiri akuheshimu na kukulipa vizuri.
Kama unalalamikia hali ya uchumi kuwa mbaya na hivyo kushindwa kupiga hatua ulizotaka kupiga unastahili kabisa kile unachopitia. Kwa sababu kwenye uchumi huo huo unaoulalamikia kuna wengine wanafanya vizuri.
Ujumbe mkuu wa kuondoka nao hapa ni kabla hujalalamikia au kulaumu chochote, angalia ni kwa namna gani unahusika na matokeo uliyopata. Utaona kwa sehemu kubwa wewe una mchango, hivyo badala ya kulaumu au kulalamika, chukua hatua kwa upande wako.
Ukifanya hivi, utajikuta unapata matokeo mazuri huku ukiwa humlaumu au kumlalamikia mwingine.
Kila unachopitia kinaweza kuwa ndani ya uwezo wako wa kukifanyia kazi au nje ya uwezo wako. Kwa kilicho ndani ya uwezo wako kifanyie kazi. Kilicho nje ya uwezo wako achana nacho.
Kulaumu na kulalamika ni kupoteza muda na nguvu zako kwa namna ambayo haitakulipa.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Normal
0
21
false
false
false
SW
X-NONE
X-NONE
/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
mso-para-margin-top:0in;
mso-para-margin-right:0in;
mso-para-margin-bottom:8.0pt;
mso-para-margin-left:0in;
line-height:107%;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,sans-serif;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;
mso-fareast-language:EN-US;}