“Since you cannot control the weather, or the traffic, or the one you love, or your neighbors, or your boss, then you must learn to control you … the one whose response to the difficulties of life really counts.” – Jim Rohn

Huwezi kudhibiti hali ya hewa,
Huwezi kudhibiti mwenendo wa uchumi,
Huwezi kumdhibiti mtu mwingine yeyote.
Yote hayo yako nje kabisa ya uwezo wako,
Lakini umekuwa unajihangaisha nayo sana.

Mtu pekee unayeweza kumdhibiti kwenye maisha yako ni wewe mwenyewe.
Maana wewe ndiye unayejijua kwa undani, ukijua nini unataka, uimara na udhaifu wako na kile kinachokusukuma.

Badala ya kuhangaika kuwadhibiti wengine, kitu ambacho kipo nje ya uwezo wako kabisa,
Hangaika kujidhibiti mwenyewe.

Jisimamie kwa umakini, jibadili tabia zinazokuwa kikwazo kwako na jisukume hasa kwenye kile unachotaka.
Uwezi wa kujidhibiti ndiyo kinachowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa.
Jidhibiti wewe mwenyewe ili uweze kufanya makubwa kwenye maisha yako.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu unacholalamikia unakistahili, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/12/09/2170

Rafiki yako anayekupenda sana.
Kocha Dr Makirita Amani.