“Courage is not having the strength to go on: it is going on when you don’t have the strength.” — Theodore Roosevelt

Wengi hufikiri ujasiri ni kuwa na nguvu ya kuendelea na mapambano pale mambo yanapokuwa magumu.
Lakini ukweli ni ujasiri ni kuweza kuendelea hata pale unapokuwa huna nguvu kabisa.
Pale unapoona huna unachoweza kufanya na ukajisukuma kufanya ndipo unapokuwa jasiri.
Na kwa kufanya hivyo unaweza kuzalisha matokeo makubwa.

Wanaofanikiwa na wanaoshindwa wote huanzia chini.
Wote huanza kuchukua hatua zinazofanana.
Lakini mambo yanapokuwa magumu, ndiyo wanapotofautiana.
Wanaoshindwa hukata tamaa na kuacha,
Wanaofanikiwa hupambana kuendelea bila ya kuacha.
Siyo kwa sababu wanajua sana, ila kwa sababu wana ujasiri, wanaweza kujisukuma hata wanapokuwa hawana nguvu kabisa ya kuendelea.

Mafanikio siyo lele mama, mafanikio yanahitaji mtu uwe jasiri kweli kweli.
Jitoke hasa kwenye kile unachofanya na kule unakotaka kufika na jiambie hutaruhusu chochote kiwe kikwazo kwako.
Kwa sababu utaendelea na safari yako bila ya kujali unapitia nini.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu wakati wa kufanya maamuzi muhimu, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/12/16/2177

Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.