“Speed is only useful if you are running in the right direction”
– Joel Barker

Kabla hujaweka juhudi kubwa kwenye kile unachofanya, hakikisha kwanza ndiyo kitu sahihi kwako kufanya.
Maana kama unachofanya siyo sahihi, juhudi zote unazoweka unazipoteza.

Kabla hujaweka kasi kubwa kwenye safari uliyonayo,
Hakikisha kwanza uko kwenye uelekeo sahihi.
Kwa sababu kama unakoelekea siyo sahihi, kuweka kasi kutakupoteza zaidi.

Kuweka juhudi na kasi siyo tatizo kwa wengi,
Ila kujua kilicho sahihi kufanya ndiyo pagumu.
Lazima mtu ujitambue, ujue unataka nini na unataka kufika wapi kisha kujua njia sahihi ya kufika unakotaka kufika.

Kila unapoianza siku yako jikumbushe yaliyo sahihi kwako kufanya.
Kila unapoanza kufanya chochote, jiulize kwanza kama ndiyo kitu sahihi kwako kufanya.
Ukifanya zoezi hili kila wakati, utatumia vizuri sana muda wako na kuweza kufanya makubwa.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu msongo wa mawazo, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/12/22/2183

Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.