“Virtue and charity start at home. If you have to go some where to display it, then it is not virtue.” – Leo Tolstoy

Upendo, wema na msaada ni vitu ambavyo vinaanzia nyumbani.
Kama unavifanya vitu hivi nje lakini huwezi kuvifanya nyumbani, siyo vya kweli.
Chochote tunachofanya kinapaswa kuanzia nyumbani, kwa wale wa karibu na wanaotuzunguka.

Kama unawapenda na kuwajali watu wa nje, lakini huwezi kufanya hivyo kwa watu wa familia yako basi huo siyo upendo, bali ni maigizo.

Ni rahisi kufanya mambo hayo kwa nje ili kuonekana na kusifiwa ila ukashindwa kuyafanya kwenye familia kwa huwa huonekani wala kusifiwa.

Upendo, wema na msaada ni vitu unavyofanya kwa sababu unajali na siyo kwa maigizo.
Hivyo vinapaswa kuanzia kwa wale watu wa karibu yako.

Mama Teresa amewahi kusema kama unataka kuibadili dunia, nenda nyumbani ukaipende familia yako
Upendo, wema na msaada vinapoanzia nyumbani, vinakuwa na nguvu kubwa kwenye dunia nzima.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu muda na nguvu, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/12/24/2185

Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.