
Bila shaka umeshatoa ushauri kwa watu wengi kwenye hali mbalimbali wanazopitia.
Labda ni mtu alipata msiba na kumpa ushauri kwamba aliyefariki amepumzika pema.
Au ni mtu aliyepata hasara au kupoteza kitu na ukamshauri kwamba kwa kuwa bado yuko hai, basi anaweza kupoteza chochote alichopata.
Cha kushangaza sasa, wewe ukiwa kwenye hali hizo hizo unataharuki, ushauri uliokuwa unawapa wengine hujipi wewe mwenyewe, unaona hali yako ni ya tofauti na ya kipekee sana.
Lakini hiyo siyo kweli, unachopitia wewe siyo tofauti na wanachopitia wengine, sema tu hisia zako zimekuwa juu zaidi.
Lakini ukitulia na kufuata ushauri wako mwenyewe, utaweza kuvuka vizuri chochote unachopitia. Kwa sababu ushauri wako ni mzuri, rahisi na wa uhakika.
Kwa chochote unachopitia na kuona unahitaji ushauri, jiulize ni ushauri gani umewahi kuwapa wengine, au kama ingekuwa mtu mwingine, ungemshauri nini. Utajipa ushauri mzuri.
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma.
Kocha