
Watu wengi wanahangaika kutafuta njia rahisi na za mkato za kupata mafanikio makubwa. Na hilo huwapeleka kufanya vitu ambavyo ni rahisi na vinavyofanywa na kila mtu. Matokeo yake ni hawafanikiwi, kwa sababu kile kinachofanywa na kila mtu hakithaminiwi. Jamii itakuthamini kama unafanya kitu ambacho inakihitaji sana, lakini hakuna mwingine anaweza au amewahi kukifanya. Watu wengi huwa wanakimbia vitu vigumu, wewe ukiviendea kwa kuangalia namna vinawanufaisha wengine, kwa kutatua changamoto zao, utaweza kupata mafanikio makubwa. Acha kukimbizana na mambo rahisi, ukishaona kila mtu anakimbilia kufanya kitu fulani, achana nacho, hakina thamani tena. Fanya kile ambacho wachache ndiyo wapo tayari kukifanya na kifanye kwa namna ambayo hakuna mwingine anaweza kufanya, huku ukitoa thamani kubwa kwa wengine na utaweza kufikia mafanikio makubwa. #NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #AfyaUtajiriHekima. Kocha.