
Kabla hujaweka juhudi kwenye chochote unachofanya, hakikisha kwanza hicho ndiyo kitu sahihi kwako kufanya. Kabla hujazidisha mbio, hakikisha uko kwenye uelekeo sahihi. Kwa sababu haijalishi ni juhudi au mbio kiasi gani unaweka, kama unachofanya siyo sahihi, unazidi kujipoteza. Siku zinaanza na kuisha na kila siku unakuwa ‘bize’ na kuchoka kweli kweli, lakini hakuna hatua unazopiga, siyo kwa sababu ni mvivu au mzembe, ila kwa sababu unachofanya siyo sahihi. Dakika chache za kuipangilia kila siku yako labla huhaianza zitakusaidia mno kuliko kuianza siku kwa mazoea na kuishia kuimalizia. Kila siku jikumbushe ndoto yako kubwa, huku ukiweka vipaumbele sahihi kwenye siku hiyo na kisha kuhangaika na hivyo tu. Juhudi hazina maana kama hujaziweka kwenye kilicho sahihi, hakikisha kila kuhudi unayoweka ni kwenye eneo sahihi. #NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma