Watu wengi ni wazito kufanya maamuzi ya maisha yao. Hiyo ni kwa sababu kufanya maamuzi ni kugumu kuliko kufuata mkumbo.

Wengi huishia kuangalia wengine wanafanya nini na kufanya pia, bila kujiuliza kama ndiyo kitu sahihi kwao kufanya.

Wewe usiwe hivyo, usiruhusu maisha yako yaendeshwe na wengine kwa namna watakavyo. Fanya maamuzi ya maisha yako mwenyewe.

Amua mwenyewe unayatumiaje maisha yako. Kuna ushawishi mwingi unaokuzunguka kuhusu kuyaishi maisha yako, wapo wanaokuambia fanya au kuwa hivi, huku wengine wakikuambia fanya au kuwa vile.

Wote hao siyo sahihi, kwa sababu hawajui nini kiko ndani yako. Wewe unajua kilicho ndani yako, unajua unachotaka, hivyo fanya maamuzi sahihi kwenye hilo.

Usiogope kusimama na wewe, ukweli hautokani na wingi, bali usahihi. Kama haupo sahihi, hata kama upo na wengi, bado haupo sahihi.

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma