
Katika kila jambo au hali unayopitia, kuwa chanya kunalipa kuliko kuwa hasi.
Kuwa chanya kunakuonesha fursa zaidi wakati kuwa hasi kunakuonesha matatizo zaidi. Kuwa chanya kunakupa matumaini wakati kuwa hasi kunakukatisha tamaa.
Pamoja na manufaa haya ya kuwa chanya, bado wengi hukimbilia kuwa hasi. Hiyo ni kwa sababu kuwa hasi ni rahisi na kila mtu anakuwa hasi.
Kuwa chanya ni kugumu, kunakutaka uende kinyume na mazoea yako, kinyume na wengi wanavyokwenda.
Na kama ilivyo kwenye mambo mengi ya maisha, kinachofanywa na wachache ndiyo kinachokupa mafanikio.
Kwa kipindi tunachoishi sasa, watu wengi wanazidi kuwa hasi kwa yale yanayoendelea. Ni wakati wa kuwa chanya kwa kila kinachoendelea na hilo litatuweka kwenye nafasi nzuri ya kupiga hatua.
Haijalishi umekutana na jambo au hali gani, kuwa chanya. Tafuta manufaa kwenye kila jambo na kila hali na pia ona hali ya uwezekano. Kuwa chanya kunalipa sana.
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma
Ni kweli Kocha, kuwa chanya ni kugumu hasa pale unapokuwa unatengenezewa mazingira fulani yanayolenga kukuonea. Lakini hamna namna itanibidi niwe chanya kwa kuangalia lilio zuri kwenye baya ili niweze kuwa na maisha tulivu.
Asante sana kwa tafakari bora.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante sana kocha kwa tafakari, watu wengi wangetamani kuwa Chanya,ila kuhitaji wepesi na kutokukubali kuwahi oka kunawafanya wengi wawe hasi,hata kama nayapitia magumu kiasi gani nitajitahidi kuwa Chanya katika maisha yangu ili niweze kuendelea kuishi kusudi la maisha yangu.
LikeLike
Vizuri Beatus
LikeLike