Kama upo njia panda na hujui kipi cha kufanya, anza kufanya chochote. Kwa kufanya chochote ni rahisi kufika kwenye kilicho sahihi kwako kufanya kuliko kuendelea kusubiri.

Kwa kuanza na chochote unajifunza na kupata msukuko wa kuendelea kuliko kusubiri. Unaweza kusubiri utakavyo, lakini tambua muda haukusubiri na muda ukishapita haurudi tena.

Unapopanga kitu, angalia wapi pa kuanzia kisha anza. Usisikilize sababu yoyote unayojipa ya kwa nini usianze, anza na chochote, ni bora kuliko kutokuanza kabisa.

Katika mambo 10 unayofanya, 8 utakosea au siyo muhimu na mawili ndiyo yatakuwa muhimu. Huwezi kujua mawili muhimu bila ya kufanya 8 yasiyo muhimu.

Kuwa mtu wa kufanya, wasemaji ni wengi, wapangaji ni wengi, ila watendaji ni wachache. Kuwa kwenye kundi la wachache na utafanya makubwa.

Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kufanya chochote ili kujua cha kufanya, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/01/11/2203

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma