Kama kuna tabia yoyote unayotaka kubadili kwenye maisha yako, anza kwa kubadili mazingira yako.

Mazingira yana nguvu kubwa kwenye kujenga na kuimarisha tabia. Angalia ni mazingira yapi unakuwepo wakati wa tabia husika.

Mfano kama unasumbuka na hasira, angalia ni wakati gani huwa unapata zaidi hasira, utagundua kuna vitu ukifanya au watu ukiwa nao inakuwa rahisi kwako kukasirika.

Ukibadili hayo, unabadili tabia. Kadhalika kwenye tabia nyingine kama ulevi au kuahirisha mambo, chunguza ni mazingira gani unakuwepo katika kutekeleza hayo na utaona wazi.

Tabia ni mazoea na mazoea huwa yanachochewa na mazingira fulani, ukibadili mazingira hayo unabadili kichocheo na tabia pia.

Ukurasa wa kusoma leo ni kila mtu anaishi kwa matumaini, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/01/18/2210

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma