
Kama kuna giza, kitu chenye manufaa unachoweza kufanya ni kuwasha mshumaa. Usihangaike kulaumu au kulaani giza, hilo halitabadili chochote.
Lakini kwa kuwasha mshumaa, unaleta mwanga ambao unaliondoa giza.
Kuna maeneo mengi yenye giza kwenye maisha yako na ya wengine, angalia ni mshumaa upi unaoweza kuwasha kisha fanya hivyo.
Kuwa chanzo cha mwanga kwenye giza, kunaleta manufaa mazuri kwa wote.
Usiwe tu mtu wa kulaumu, kulaani na kulalamika, badala yake kuwa mtu wa kuchukua hatua.
Ukurasa wa kusoma ni kuhusu unachozalisha, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/01/26/2218
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma
Nitawasha mshumaa pale kwenye giza bila kulalamika
LikeLike
Safi sana.
LikeLike