Watu wamekuwa wanatumia njia zisizo sahihi ili tu kupata matokeo wanayoyataka.

Wakiamini kilicho muhimu ni matokeo na siyo njia iliyoleta matokeo hayo. Wanaamini matokeo yakiwa mazuri basi njia itakuwa sahihi.

Lakini hilo siyo kweli, tumeona wengi wakianguka baada ya kupata matokeo waliyotaka kwa sababu njia walizotumia hazikuwa sahihi.

Hakikisha unaanza na njia sahihi na kukaa kwenye njia sahihi, matokeo utakayoyapata yatakuwa sahihi na kudumu kwa muda mrefu.

Matokeo hayahalalishi njia, kama njia siyo sahihi, matokeo hayawezi kuwa sahihi.

Ushindi wowote unaoutafuta kwenye maisha yako, tumia njia zilizo sahihi.

Ukurasa wa kusoma ni kuhusu tatizo la mawasiliano ya mbali, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/01/26/2219

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma