
Kila uovu unaofanyika, huwa unaanzia kwenye uongo. Tena uongo unaanza kidogo, lakini unaendelea kukua ili kulinda uongo wa mwanzo.
Lakini pia mtu anapotumia uongo na ukamfanikishia kile anachotaka, anashawishika zaidi kuendelea na uovu mwingine.
Wengi huanza na uongo kidogo, wakijiambia hawataendelea hivyo, lakini uongo huo unapowapa wanachotaka, wanajikuta wakiendelea nao ili kuwa na msimamo.
Ni msimamo ndiyo unaomfanya mtu azidi kuzama kwenye uongo na kufanya maovu makubwa.
Kama unataka kujiepusha na maovu, anza kuukataa uongo, epuka kutumia uongo hata kama ni mdogo na hapo utaweza kusimama na yaliyo sahihi.
Ukurasa wa kusoma ni kuhusu namba za ajabu, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/01/30/2222
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma
Asante Sana kocha, kukataa uongo ni kujiepusha na maovu yote.
LikeLike