Ni rahisi kusema unatekeleza tu wajibu wako bila kujali nini kinatokea kwa wengine.Ni rahisi kujali maslahi yako bila ya kujali ya wengine. Inashawishi kupambana na hali yako na kuwaacha wengine wapambane na hali zao.Hayo yanaweza kukupa kile unachotaka, yanaweza kukufanya ubaki kwenye kazi yako, lakini hayatakufanya uache alama yoyote.Hakuna anayekumbukwa kwa yale aliyopata, kwa maslahi yake aliyojitimizie, bali watu hukumbukwa kwa namna walivyogusa maisha ya wengine.Hakuna aliyeridhika kwa kujiangalia yeye tu, bali walioridhika waliwaangalia na wengine pia.Kwa kila unachofanya, angalia ni kwa namna gani unagusa maisha ya wengine, namna gani unayafanya kuwa bora zaidi.Weka hilo mbele na maisha yako yatakuwa na mchango bora kwa wengine, huku wewe ukiridhika pia.Ukurasa wa kusoma ni kuhusu kutokujichukulia poa, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/02/06/2229#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma