Hakuna anayekosa usingizi kwa kukufikiria wewe, kila mtu anahangaika kujifikiria mwenyewe.

Unafikiria wengine wanafikiri nini kuhusu wewe, kumbe na wao wanafikiria wewe unafikiri nini kuhusu wao.

Unaweza kuacha kufanya baadhi ya vitu ili kuwaridhisha wengine kumbe hata hawana muda wa kufuatilia nini umefanya na kwa nini umefanya.

Kila mtu ana changamoto anazopambana nazo kwenye maisha yake, anazipa hizo kipaumbele kabla ya mengine yote.

Kwa kujua hili unapaswa kuwa huru, kuchagua kuyaishi maisha yako badala ya kujaribu kuwaridhisha wengine.

Maisha yako ni yako, yaishi kwa ukamilifu wake.

Ukurasa wa kusoma ni kuhusu kujishikiza na kusudi badala ya matokeo, soma; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/02/07/2230

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma