Watu hufikiri kuna kazi au biashara ukizifanya mafanikio ni uhakika. Hilo siyo kweli, kwenye kila kazi na biashara, kuna waliofanikiwa na walioshindwa.

Kinachowatofautisha watu hao ni sifa zao za ndani. Wale wanaofanikiwa wana sifa za tofauti kabisa na wanaoshindwa. Sifa za mtu zina nguvu na mchango mkubwa mno kwenye mafanikio yake.

Tabia alizonazo mtu, iwe anazijua au hazijui, ndiyo zenye nguvu ya kuamua mafanikio atakayoyapata. Ni muhimu sana kuwa mtu sahihi, mwenye sifa na tabia sahihi ndiyo uweze kufanikiwa.

Kuwa na nidhamu ya hali ya juu, kujituma sana, kuwa na uadilifu na kutokukata tamaa ni sifa muhimu kwenye mafanikio. Kuwa mtu wa kujifunza na kujaribu mambo mapya ni tabia zitakazokufikisha mbali.

Hakikisha unakuwa mtu sahihi na mafanikio utayapata bila ya kujali unafanya nini.

Ukurasa wa kusoma ni kuhusu kupumzisha akili, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/02/09/2232

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma