Ustaarabu unajengwa kwenye msingi wa uaminifu, pale watu wanapoweka ahadi na kutekeleza ahadi hizo. Uaminifu unapokosekana, watu hawaaminiani na kila mtu anaumia.

Unaenda kwa daktari ukiamini atafanya kile chenye manufaa kwako, kadhalika kwa mwalimu, mwanasheria, mhasibu na hata mfanyabiashara.

Swali la kujitafakari leo ni je, ahadi gani unawapa watu na kujisukuma kuitekeleza? Kwa sababu wote waliofanikiwa kwa kiwango kikubwa, waliahidi makubwa na kuyatekeleza. Wakati wale walioshindwa wakiahidi na kutokutekeleza.

Kipi kikubwa unachowaahidi wengine na kujisukuma kutekeleza? Anzia hapo.

Ukurasa wa kusoma ni hofu ya kifo inavyokuwekea ukomo kwenye maisha, soma; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/02/10/2233

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma