Pesa ni nyenzo inayokuwezesha kupata muda na nguvu zaidi. Kama kuna kitu unafanya mwenyewe kwa masaa 10 kwa siku, ukitumia pesa unaweza kupata wengine wanaokupa masaa hayo kumi na nguvu zaidi.

Wengi wamekuwa wanajisifia kwa kuokoa pesa, kabla hawajaangalia ni kuda na nguvu kiasi gani wanapoteza. Mara zote unaookka pesa, jua kabisa unapoteza muda zaidi.

Hivyo jua vipindi vya maisha yako na kuchagua kwa usahihi, wakati ambao huna pesa, tumia muda na nguvu zako kupata pesa zaidi. Na wakati una pesa, tumia pesa hizo kupata muda na nguvu zaidi ili uweze kupata pesa nyingi zaidi.

Usitumie muda kuokoa pesa, badala yake tumia pesa kuokoa muda. Maana muda una ukomo, wakati pesa haina ukomo wowote.

Ukurasa wa kusoma ni kuhusu wawakilishi wa jamii zetu, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/02/13/2236

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma