Kwa malengo na mipango uliyonayo, hapo ulipo tayari una vitu vingi unavyoweza kuanza kufanya. Lakini wengi huwa hawaanzi, badala yake wanatafuta sababu za kwa nini hawawezi kuanza.

Kila mtu huwa anapata kile anachotafuta, anayetafuta sababu za kutokufanya kitu anazipata na anayetafuta mahali pa kuanzia anapapata.

Wewe unataka nini, kama ni kuanza, weka sababu pembeni na tafuta wapi unaweza kuanzia, na utapaona vizuri tu.

Hakuna asiye na pa kuanzia, inategemea mtu anatafuta nini.

Ukurasa wa kusoma ni kuhusu kuepuka gereza walipo wengi, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/02/16/2239

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma