Sisi binadamu tuna uwezo mkubwa wa kumsoma mtu kupitia anachosema, jinsi anavyokisema na kile anachofanya.

Hivyo kila unachofanya na kusema, kuna ujumbe unatuma kwa wengine, ambao wanausoma vizuri na kuamua wewe ni mtu wa aina gani.

Mtu anapokuhudumia unajua kabisa kama mtu huyo anakujali au la, kama anapenda anachofanya au la. Huhitaji akuambie, utajua hilo kwa namna anavyokuhudumia.

Kwa kujua hili, tunapaswa kuwa makini sana kwa tunayosema na kufanya, siyo tuigize, bali tuwe halisi na tuweze kutuma ujumbe sahihi kwa wanaotuzunguka.

Ukurasa wa kusoma ni kuhusu sababu za biashara kufa, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/02/18/2241

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma