Dunia haikusubiri wewe mpaka uwe tayari kuanza. Kila siku jua linachomoza na kuzama, miaka inayoyoma na muda wako hapa duniani unazidi kupungua.

Wakati unapanga kusubiri au kuahirisha chochote, jikumbushe hili.

Unaweza kufa muda wowote, jua hilo na likusaidie kwenye kuyaishi maisha yako ya kila siku, ndivyo alivyosema na kuishi Mstoa Marcus Aurelius.

Tuishi kwa msingi huu pia, leo na kila siku na tutatumia vizuri muda tulionao.

Ukurasa wa kusoma ni kuhusu wewe kukosea, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/02/19/2242

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma