Vitabu vya dini huwa vinasema dhambi zote zinalingana, kwamba hakuna dhambi kubwa wala ndogo.
Hilo ni kweli kwa sababu kosa ni kosa na kama kitu siyo kweli basi siyo kweli, haimaanishi ni kikubwa au kidogo.
Lakini kuna dhambi au makosa ambayo mtu akiyafanya, pamoja na kuwa amekosea, basi kuna manufaa anakuwa ameyapata.
Mfano kama una njaa na ukaona chakula ukakiiba ili ule kutuliza njaa yako, hilo ni kosa, lakini lina manufaa kwako, njaa ilikuwa kali na umeweza kuituliza.
Katika dhambi na makosa mengi watu wanayofanya, kuna matatu ambayo hayana faida yoyote ile kwa anayeyafanya, hivyo yanamsumbua kufanya na yanasumbua nafsi yake kwa kujua amefanya.
La kwanza ni hasira, hakuna mtu amewahi kunufaika kwa namna yoyote ile kupitia hasira, badala yake wengi hujikuta wakifanya mambo yanayowaumiza au wanayokuja kuyajutia kutokana na hasira.
La pili ni chuki, kumchukia mtu yeyote yule bila ya kujali amefanya nini, haijawahi kumsaidia yeyote, badala yake inamfanya mtu ajichukie yeye mwenyewe. Kwa sababu chuki yoyote unayopeleka kwa mwingine, inarudi na kwako pia.
La tatu ni kinyongo, kumwekea mtu kinyongo ni mateso makubwa kwako, ni sawa na kujitonesha kidonda ambacho mtu amekuumiza, ukiamini yeye anaumia. Unajiumiza zaidi mwenyewe kwa kinyongo chochote unachokuwa umejiwekea.
Simaanishi makosa mengine ni sahihi kufanya na wala sisemi haya ndiyo makosa yasiyo na manufaa pekee, bali nimekuwa naona watu wakiyarudia makosa haya kila wakati, huku wakiwa hawapati manufaa yoyote yale.
Achana na makosa haya matatu mara moja na usiyape nafasi kabisa kwenye maisha yako.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Asante Sana kocha kwa dhambi hizi tatu zisizo na faida.
LikeLike
Karibu Godius.
LikeLike
Asante Sana kocha, makosa haya matatu ni ya kuyaacha mara moja. Shukrani
LikeLike
Vizuri Stephano.
LikeLike
Asante Sana kocha nitaendelea kuyawekea umakini haya mambo matatu hasira,chuki,kinyogo, nahitaji furaha na Amani ktk maisha yangu.
LikeLike
Vizuri Beatus
LikeLike