Kwanza ni lazima uwe na mtazamo mkubwa kuliko tatizo lenyewe, lazima ufikiri kwa ukubwa kiasi kwamba tatizo linaonekana ni dogo. Kwa sababu usipofanya hivyo, tatizo litaonekana ni kubwa kuliko uwezo wako.

Pili inabidi ujitofautishe na tatizo hilo, uweze kuliona kama vile mtu mwingine anavyoweza kuliona, uache kujishikiza nalo kihisia. Hisia zikishaingia kwenye tatizo huonekana ni kubwa na lisilowezekana.

Tatu angalia padogo pa kuanzia, ukiliangalia tatizo zima hutaona cha kufanya, ila ukiangalia padogo unapoweza kuanzia, utaweza kuanza na kupiga hatua katika kulitatua tatizo hilo.

Hakuna tatizo ambalo ni kubwa na linaloshindikana kabisa, bali mtazamo na fikra zetu ndiyo zinayafanya matatizo yaonekane hivyo. Badili mtazamo wako juu ya matatizo, usikubali hisia zako ziingilie kwenye matatizo hayo na ligawe tatizo kwenye sehemu ndogo ili upate pa kuanzia.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha