
Unaweka mipango yako vizuri, unafanya kila unachopaswa kufanya lakini matokeo yanakuja tofauti na ulivyotegemea.
Hapo ndipo wengi huvurugwa na kukata tamaa, kwa kuona mambo hayawezekani.
Unapaswa kujua hiyo ni hali ya kawaida, inayomkumba kila mtu.
Hata unaoona wamefanikiwa sana, siyo kwamba hawakutani na hali hiyo, wanakutana nayo sana, ila wanaikabili kwa kuwa watulivu na kuweza kuona hatua sahihi za kuchukua.
Ukishavurugwa, hisia zinakutawala na huwezi kuchukua hatua sahihi. Ukiwa na utulivu unaweza kufikiri kwa usahihi na kuchukua hatua sahihi.
Falsafa ya Ustoa ina manufaa makubwa katika hali kama hizo, kwa kuwa inatukumbusha umuhimu wa kuwa na utulivu na kutoruhusu hisia zitutawale wakati wa kufanya maamuzi.
Falsafa hii inatukumbusha tunachoona siyo uhalisia bali fikra zetu ndiyo zinapelekea tuone hivyo.
Ukurasa wa kusoma ni kuhusu dhambi zisizo na faida; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/02/21/2244
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma