
Wengi hufikiri ili kufanikiwa lazima mtu afanye mambo mengi, ahangaike na kila linalopita mbele yake.
Lakini huo siyo ukweli, wale wanaohangaika na mengi huwa hawafanikiwi, kwa sababu wanatawanya sana nguvu zao.
Ili ufanikiwe unapaswa kufanya mambo machache kwa kina na siyo kufanya mengi kwa juu juu.
Kufanya hayo machache kunakuweka kwenye utulivu unaohitajika ili ufanikiwe.
Jua ni mambo yapi machache unayoweza kuyafanya vizuri na kwa utofauti kabisa na wengine, kisha weka juhudi kubwa katika kuyafanya hayo na jipe muda, mafanikio lazima uyapate.
Ukurasa wa kusoma ni kuhusu kutatua matatizo makubwa, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/02/22/2245
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma
Asante sana kocha
LikeLike