
Matatizo na changamoto kubwa zinazokusumbua kwenye maisha yako ni chache na zinazojirudia rudia.
Matatizo na changamoto zinazowakabili wanadamu ni zile zile ambazo zimekuwepo miaka na miaka.
Hivyo usihangaike na matokeo, badala yake tafuta chanzo. Na pia suluhisho bora ni suluhisho la zamani, ambalo limekuwepo miaka na miaka.
Usikubali kuendelea kusumbuka na matatizo yale yale maisha yako yote, nenda kwenye chanzo cha tatizo na tumia njia sahihi kulitatua.
Uzuri ni kwamba wewe siyo wa kwanza kupitia chochote unachopitia, wengi walishapitia na wakavuka vizuri, jifunze kwao ili na wewe uvuke pia.
Ukurasa wa kusoma ni wewe siyo wa kwanza kupitia, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/03/16/2267
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma