Hakuna chochote kinachoweza kuhalalisha uongo, iwe unatumika kwa nia njema, matokeo yake huwa ni mabaya.

Ni ukweli pekee ulio sahihi na unaomuweka mtu huru. Yeyote anayeweza kutumia uongo mdogo, anaweza kutumia mkubwa pia.

Unapotumia uongo kwa sababu unaona ukweli utawaumiza watu, unaishia kuwaumiza zaidi.

Ukweli hata ufichwe kiasi gani, haubadiliki, utabaki kuwa ukweli na kama ulifichwa kwa sababu unaumiza, utaendelea kuumiza zaidi.

Mara zote simama kwenye ukweli, unaweza kuumiza, lakini unakuweka huru.

Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kujenga uaminifu, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/03/18/2269

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma