
Matokeo unayopata sasa kwenye maisha yako, siyo ajali wala bahati, bali ni wewe mwenyewe umeyatengeneza.
Umeyatengeneza kutokana na kile unachojua na hatua ambazo umekuwa unachukua.
Kama unataka kupata matokeo ya tofauti na unayopata sasa, kwanza jifunze vitu vya tofauti na kisha chukua hatua za tofauti.
Albert Einstein aliwahi kunukuliwa akisema ujinga ni kufanya kitu kile kile kwa namna ile ile na kutegemea matokeo ya tofauti.
Usikubali kuwa mjinga, jua kipi cha tofauti unataka, jifunze kwa kina kuhusu kitu hicho na chukua hatua zitakazokufikisha kwenye kitu hicho.
Ukurasa wa leo ni jinsi ya kuzuia matusi yasikuumize, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/03/21/2272
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma
Hakika hiki ni kisima kwa maana ya halisi ya kabisa ya kupata Maarifa sahihi.
LikeLike
Asante Beatus
LikeLike