2280; Kila kitu kinaanza na mteja…
Watu huwa wanahangaika na mambo mengi kwenye biashara zao, ambayo hata siyo muhimu.
Yale ya muhimu kabisa na yanayoiwezesha biashara kupiga hatua huwa hayapewi uzito mkubwa.
Watu huhangaika na wazo, jina, mtaji, eneo na mengine, lakini mteja hawampi kipaumbele kikubwa.
Watu huhangaika na mbinu za kila aina, ila mteja siyo kitu kinachowahangaisha.
Kama unataka mafanikio kwenye biashara yoyote ile unauoifanya, unapaswa kuanza na mteja.
Na kila unachofanya kwenye biashara, kianze na mteja kwanza.
Maswali yote unayojiuliza kuhusu biashara, majibu yake yanaanzia kwa wateja.
1. Ni wazo gani zuri la biashara itakayokupa mafanikio?
Jibu; kile ambacho watu wanaokuzunguka au unaoweza kuwafikia wanakihitaji na wako tayari kulipia kukipata.
2. Nawezaje kupata faida zaidi kwenye biashara yangu?
Jibu; kwa kuongeza wateja zaidi unaowahudumia.
3. Nawezaje kuongeza wateja zaidi kwenye biashara?
Jibu; kwa kuwahudumia vizuri sana wale ulionao sasa na kuwaomba wakuletee wateja wengine.
Haijalishi ni swali gani unajiuliza, jibu tayari lipo kwa wateja wako, anzia kwao na utaona kilicho sahihi kufanya.
Unapofanya biashara, bosi wako wa kwanza ni mteja, hivyo unapaswa kumpa kipaumbele anachostahili kupewa.
Angalia tatizo ambalo tayari watu wanalo na wanatafuta sana suluhisho.
Njoo na suluhisho ambalo wanaweza kulimudu na wapatie.
Wahudumie vizuri unaoanza nao kiasi cha wao kuwa tayari kuwaleta wengine.
Mchakato wote huo unahitaji kazi, muda na uvumilivu, lakini utakupa matunda makubwa.
Usihangaike na yasiyo muhimu.
Kocha.
Asante kwa somo zuri
LikeLike
Karibu.
LikeLike