
Falsafa kuu ya mafanikio inayotuongoza kwenye safari nzima ni upendo.
Kwa kujipenda sisi wenyewe tunajikubali tulivyo na kuwa sisi, badala ya kutaka kuwa kama wengine.
Kwa kuwapenda wengine tunawakubali na kuwapokea walivyo na kuona njia bora ya kushirikiana nao, bila kutaka wawe tofauti.
Kwa kupenda kile tunachofanya hakiwi tena kazi kwetu bali mchezo na tunakuwa tayari kukifanya kwa muda mrefu kuliko wengine wote.
Simama kwenye upendo kama unayataka mafanikio makubwa.
Ukurasa wa kusoma ni kuanza na mteja; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/03/29/2280
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma
Barikiwa sana kocha kwa tafakari bora.
LikeLike
Asante.
LikeLike