
Wafanye watu wakuchague wewe kutokana na uwezo ulionao katika kufanya vizuri kile wanachohitaji na siyo kwa kukuonea huruma.
Wakikuchagua kwa huruma wanakuwa wametumia hisia, ambazo huwa hazidumu.
Lakini wakikuchagua kwa uwezo, wanakuwa wametumia mantiki, ambayo hudumu wakati wote.
Badala ya kutaka uonewe huruma au upendelewe, kazana kujijengea uwezo wako kwa kufanya makubwa na kutoa thamani kubwa kwa wengine.
Kwenye kazi au biashara, fanya yale ambayo hakuna anayeweza kufanya na yanayoongeza thamani kwa wengine na utachaguliwa au kukubaliwa kwa uwezo wako huo.
Ukurasa wa kusoma ni kuwa sahihi ni kukosea; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/03/31/2282
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma