Kama unachotaka ni kubembelezwa, umeshapishana na mafanikio. Kama hutaki kabisa kuumia, huwezi kuyafikia mafanikio makubwa.

Hatua ya kwanza ya kufanikiwa ni kusimama kwenye ukweli na ukweli huwa unaumiza.

Uongo unaweza kukubembeleza, ila ni kwa muda tu, ukweli utakuumiza, lakini utakuweka huru.

Mara zote simama kwenye ukweli, ndiyo njia pekee ya kuwa wewe na kifika kwenye mafanikio makubwa.

Ukurasa wa kusoma ni kusikia unachotaka kusikia; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/04/16/2298

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma