
Kama mtu ana kitu ambacho watu wengi wanakihitaji na hawawezi kukipata pengine, huyo ana nguvu ya kukiuza kwa namna anavyotaka yeye.
Kama watu wanaweza kupata wanachotaka popote, wana nguvu ya kuchagua wakapate wanachotaka wapi.
Mwenye machaguo mengi ndiye mwenye nguvu ya kuamua apate kiasi gani kwenye majadiliano yoyote yale.
Kama unataka kujijengea nguvu hii, hakikisha unakuwa na machaguo mengi.
Na njia ya kuwezesha hilo ni kwa kutoa thamani kubwa ambayo watu hawawezi kuipata pengine isipokuwa kwako.
Ukurasa wa kusoma ni wanachokulipa ndiyo thamani yako; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/04/25/2307
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma