
Unaweza kuwa bize kweli kweli, kila siku unachoka sana, lakini unayofanya yakawa ni kikwazo kwa unachotaka.
Hili ndiyo linazuia wengi wasifanikiwe, wanahangaika na mambo ambayo siyo tu hayawasaidii, bali pia yanawazuia wasipate wanachotaka.
Kila unachofanya, jiulize kwanza kama kitakufikisha unakotaka na kuwa na ushahidi kutoka kwa wale ambao wameshafika unakotaka wewe na kuona kama walifanya hivyo pia.
Usifanye kitu chochote kwa kufuata mkumbo, maana wengi huendesha maisha yao kwa mazoea wasijue madhara ya yale wanayofanya.
Jikumbushe kila unachofanya kinaweza kuchangia kupata unachotaka au kukukwamisha.
Fanya yanayokupeleka unakotaka, achana na yanayokukwamisha.
Ukurasa wa kusoma ni vitu vya kushangaza; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/04/27/2309
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma