
Kuna watu falsafa yao ya kutafuta fedha ni wanachoangalia ni kama fursa inaingiza fedha, hawajali fedha hizo zinapatikanaje, wao kama kitu kina faida wanafanya.
Watu hawa hujikuta wananasa kwenye fursa ambazo zinaingiza faida kubwa siyo kwa sababu zina thamani ambayo watu wananufaika nayo, bali kwa sababu zina uhaba.
Kwa uhaba wake, wengi wanakimbilia kununua siyo kwa sababu wana matumizi, ila kwa sababu wanategemea bei ipande zaidi na wapate faida.
Na inaenda hivyo mpaka bei inapofika kiwango ambacho haiwezi kwenda tena na inaanza kuporomoka na hapo ndipo wengi wanapoumia.
Unapotaka kujenga utajiri mkubwa na utakaodumu, usiangalie tu kinachokupa faida, angalia pia faida hiyo inatokana na nini. Faida nzuri ni inayotokana na thamani na siyo uhaba pekee.
Kwenye huu ukurasa unajifunza kwa kina zaidi kuhusu hilo; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/13/2325
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma