
Maumivu ni sehemu ya kawaida kwenye maisha yetu hapa duniani. Mambo huwa hayaendi kama tunavyotaka sisi na hilo huleta maumivu.
Lakini mateso kwenye maisha ni kitu ambacho mtu unakichagua mwenyewe. Unachagua mateso pale unapokataa kukubaliana na ilichotokea na ambacho kipo nje ya uwezo wako au unapolazimisha kitu kiende unavyotaka wewe.
Mateso hayo ya kutengeneza huwa ndiyo chanzo cha msongo na mvurugo wa maisha. Ukichagua kutokuteseka, unakuwa umechagua kuondokana na msongo kwenye maisha.
Maisha tayari ni magumu, usiyafanye kuwa magumu zaidi kwa kujitengenezea mateso, kubali kilicho nje ya uwezo wako na usilazimishe kila kitu kiwe kama unavyotaka wewe.
Ukurasa wa kusoma ni vyanzo viwili vya msongo; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/16/2328
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma