Mawazo 10 ya kuingiza kipato kupitia uandishi wa vitabu.

Huwa nasema kila mtu ni kitabu kinachotembea.
Maisha uliyoishi mpaka sasa kuna mengi umejifunza na kupitia ambayo ukiweka kwenye maandishi wengine wanaweza kukifunza pia.

Pamoja na uandishi kuwa njia ya kushirikisha uzoefu wako kwa wengine, pia ni njia ya kuingiza kipato.
Na hapa kuna mawazo kumi ya kuingiza fedha kupitia uandishi wa vitabu.

  1. Kuuza vitabu ulivyoandika.

  2. Kutengeneza kozi kutoka kwenye kitabu na kuiuza.

  3. Kuwa mnenaji kwenye makongamano mbalimbali na kulipwa.

  4. Kuuza haki za wengine kutumia kitabu kwa njia nyingine kama kukitafsiri kwa lugha nyingine, kukigeuza kuwa muvi n.k.

  5. Kutumia kitabu kutangaza bidhaa na huduma zako nyingine.

  6. Kushauri na kusimamia wengine kwenye uandishi wa vitabu kwa kutumia uzoefu wako.

  7. Kukuza mtandao wako na kuutumia kupata fursa za kuingiza kipato zaidi.

  8. Kujenga mamlaka (authority) na hivyo kuaminika zaidi kitu kinachokupa fursa zaidi.

  9. Kuwaandikia wengine vitabu (ghost writing).

  10. Kutoa mafunzo ya uandishi wa vitabu.

  11. Kuhariri vitabu vya watu wengine.

Ipo kauli kwamba katika zama hizi, kitabu ndiyo business card, yaani watu watakujua kupitia kitabu chako.
Hivyo kuandika kitabu kunakupa fursa nyingi sana.

Kocha.