
Kwenye maisha yako utakutana na watu wenye imani na itikadi kali juu ya kitu ambacho unajua kabisa siyo sahihi.
Ushahidi uko wazi kabisa kwamba wanachoamini watu hao siyo sahihi, lakini bado wanakiamini na kukisimamia.
Unaweza kuona ni wajibu wako kuhakikisha unawashawishi waachane na imani hizo, lakini utakuwa umefanya makosa sana ukilazimisha hilo. Maana utapoteza muda na nguvu zako na hakuna matokeo mazuri utakayoyapata.
Unapaswa kuwa na ukomavu wa kiroho wa kuweza kuwakubalia watu kile wanachoamini hata kama wanakosa kama hakina madhara kwako.
Lazima uweze kupuuzia ujinga na makosa mbalimbali ya watu yanayotokana na imani au itikadi zao kama unataka maisha tulivu.
Kumbuka wewe siyo kiranja wa dunia, hata kama unajua ukweli ni upi, siyo wote wapo tayari kuupokea. Hivyo wapime vizuri wote unaojihusisha nao kabla hujapoteza muda na nguvu zako kwa mambo ambayo hawatabadilika.
Ukurasa wa kusoma; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/28/2340
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma