Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia soko la hisa…

Wengi wanaposikia hisa huwa wanaona ni kitu kikubwa na wasichoweza kujihusisha nacho kwa sababu hawana uelewa.

Lakini siyo kitu chenye ukubwa wa kutisha, yeyote anaweza kujifunza na kulielewa soko la hisa kisha kulitumia kuingiza kipato.

Hapa kuna njia kumi za kuingiza kipato kupitia soko la hisa.

  1. Kuwa mwekezaji wa kununua hisa na kukaa nazo kwa muda mrefu ili ziongezeke thamani.

  2. Kuwa mchuuzi wa kuuza na kununua hisa pale bei zinapobadilika.

  3. Kuwasaidia wengine kufanya uwekezaji kwenye soko la hisa.

  4. Kuwa na blog inayohusu mambo ya hisa na kuingiza kipato kupitia matangazo.

  5. Kuandika kitabu kinachohusu mambo ya hisa.

  6. Kuwa mshauri wa wengine kuhusu mambo ya hisa na mwenendo wa soko.

  7. Kuanzisha mfuko wa pamoja wa uwekezaji (hedge fund) na kuwaalika wengine kuweka mtaji wa kuwekeza kisha kulipwa kulingana na mtaji unaowekezwa.

  8. Kuandaa ripoti za uchambuzi wa mwenendo wa soko la hisa na kuziuza.

  9. Kuwa mnenaji kwenye makongamano mbalimbali kwenye eneo la hisa na kulipwa.

  10. Kuwa na vipindi vya sauti na video vya kurushwa mtandaoni kisha kulipwa kwa matangazo au wadhamini.

Kadiri wengi walivyo na uelewa na kuliogopa soko la hisa, ndivyo fursa zinakuwa nyingi kwako katika kuwafundisha na kuwasaidia kuwekeza.
Tumia njia hizi na nyingine kuingiza fedha kupitia soko la hisa.
Kabla hujatumia njia yoyote katika hizo, lazima ujifunze na kulielewa soko kwa kina.
Pia lazima ujipe muda kujijengea ubobezi kabla hujategemea kupata malipo makubwa kwenye njia hizo.

Kocha.