
Kama unatafuta sababu za kutokufanya kitu, utazipata nyingi tu. Na kama unatafuta njia ya kufanya kitu, utazipata za kutosha.
Akili yako ina uwezo mkubwa wa kuvuta kwako kile unachotaka. Hivyo kama hujapata unachotaka, hebu anza kwa kuangalia akili yako inatafuta nini zaidi na utagundua kila ulichonacho sasa ndiyo akili yako imekuletea.
Huwezi kuilaumu sumaku kwa kunasa chuma, ndiyo kitu inatafuta. Akili yako ni kama sumaku, inavuta kwako kile unachotaka sana, kile unachofikiria kwa muda mrefu. Kwa kujua haya, itumie akili yako vyema.
Ukurasa wa kusoma ni muda sahihi wa kufanya kitu muhimu; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/06/04/2347
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma