2347; Muda sahihi wa kufanya kitu kikubwa…

Haujawahi kuwepo,
Hakuna wakati utakaosema uko tayari kufanya kitu ambacho ni kikubwa.

Kila wakati utaona unahitajika kusubiri zaidi kwa sababu muda bado haujawa sahihi.
Iwe ni kuanzisha biashara, kubadili kazi au kuanza mradi wowote mkubwa, utaona bado muda haujawa sahihi.

Hupaswi kuruhusu hili liwe kikwazo kwako, badala yake unapaswa kulitumia kama kiashiria.
Unapojiona hujawa tayari kufanya lile unalojua ni muhimu kufanya, jua hofu ndiyo inakufanya uone hujawa tayari.

Tambua hofu hiyo, pima hatari zinazozalisha hofu hiyo na kisha chukua hatua sahihi.
Tambua ingekuwa rahisi isingekuwa vigumu kwako kufanya, hivyo kazana kufanya kwa sababu ni kitu chenye manufaa kwako.

Muda sahihi wa kufanya chochote kikubwa ni sasa au hutafanya kabisa.
Hakuna wakati mwingine ambao utakuwa tayari zaidi ya ulivyo sasa.

Kama ni muhimu basi fanya.

Kocha.