Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia mgahawa.
Chakula ni hitaji la msingi la watu na wataendelea kula kila siku ya maisha yao.
Biashara ya mgahawa ni biashara yenye uhitaji mkubwa, lakini yenye changamoto kubwa pia.
Hapa kuna mawazo 10 ya kuingiza kipato zaidi kwenye biashara hiyo ya mgahawa.
- Kuuza chakula kwa wateja wanaofika kwenye mgahawa.
-
Kusambaza chakula kwenye maofisi au majumba ya watu.
-
Kutoa huduma za chakula kwenye shughuli mbalimbali kama sherehe, mikutano n.k.
-
Kuwa na migahawa mingi kwenye maeneo mbalimbali.
-
Kuwa na kanuni yako ya mapishi (recipe) ambayo unaiuza kwa wengine.
-
Kutoa leseni kwa wengine kuendesha mgahawa kwa kutumia jina na kanuni zako za mapishi (franchise).
-
Kununua na kutumia jina na kanuni za wengine za mapishi.
-
Kuandika kitabu cha kanuni mbalimbali za mapishi au jinsi ya kuendesha mgahawa.
-
Kuandaa kipindi cha mapishi na kurusha kwenye tv au youtube kisha kuingiza kipato kupitia matangazo au wadhamini.
-
Kuwafundisha wengine mapishi na uendeshaji wa migahawa kwa kulipia mafunzo hayo.
Biashara ya mgahawa ina fursa nyingi ambazo mtu anaweza kufanyia kazi. Na kama nilivyoeleza hapo juu, changamoto zake ni nyingi pia, hivyo lazima uweke juhudi na umakini mkubwa.
Kocha.