Mawazo 10 ya kuingiza fedha kwenye ujenzi.
Makazi ni hitaji la msingi kabisa la watu. Watu wanahitaji mahali pa kukaa. Hili linatoa fursa nyingi kwenye sekta ya ujenzi.
Hapa kuna mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia sekta ya ujenzi.
- Kujenga nyumba na kuzipangisha kwa watu.
-
Kujenga nyumba na kuziuza.
-
Kuuza vifaa vya ujenzi.
-
Kuwa na kampuni ya ujenzi inayochukua tenda mbalimbali za ujenzi.
-
Kusimamia majengo ya wengine kwenye kuuza au kupangisha.
-
Kununua nyumba, kuzifanyia maboresho na kisha kuziuza.
-
Kununua majengo yanayopigwa mnada na kuyaboresha kisha kupangisha au kuuza.
-
Kutumia majengo uliyonayo kupata mkopo kutoka taasisi za kifedha.
-
Kuwa na majengo kwa ajili ya hoteli.
-
Kuwa wakala au dalali kwenye sekta ya ujenzi kwa kutafuta wateja kwa ajili ya kupanga au kununua majengo mbalimbali.
Fursa hizi za kwenye sekta ya ujenzi zinaweza kufanyiwa kazi na yeyote. Zinahitaji muda ili mtu uweze kujijenga vizuri kibiashara na ukishakomaa kipato kinakuwa kizuri.
Kocha.