Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia biashara ya mbao.

Samani mbalimbali zinatengenezwa kwa kutumia mbao. Hilo linafanya uhitaji wa mbao kuwa mkubwa na kutoa fursa ya kibiashara kwa wale wanaoweza kushughulika na upatikanaji wa mbao.

Hapa ni mawazo 10 ya kuingiza kipato kupitia biashara ya mbao.

  1. Kununua na kuuza mbao kwa reja reja.

  2. Kununua na kuuza mbao kwa jumla.

  3. Kuwa na shamba la miti ya mbao ba kuiuza miti au kuchana mbao na kuziuza.

  4. Kununua shamba la miti, kuchana mbao na kuziuza.

  5. Kuwa na mashine za kuchana miti ya mbao.

  6. Kusafirisha mbao na kupeleka maeneo yenye uhitaji zaidi.

  7. Kuwa na mashine za kutengeneza mbao kwa miundo mbalimbali ya samani.

  8. Kuwa na karakana inayofanya kazi za mbao.

  9. Kuwa fundi anayetengeneza samani za kutumia mbao.

  10. Kuwa dalali kwenye mbao, kuwaunganisha wateja na wazalishaji wa mbao.

Kama upo au unapanga kuingia kwenye biashara ya mbao, angalia njia hizi na nyingine unazoweza kufikiria ili kuongeza wigo wako wa kuingiza kipato.

Kocha.