Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia biashara ya nguo.
Hakuna siku watu watatembea uchi duniani, hivyo mavazi yanabaki kuwa hitaji la msingi kabisa kwa wanadamu.
Japo ni biashara yenye changamoto kubwa ya ushindani, maana wengi huona ndiyo biashara rahisi kwao kuingia na kufanya.
Hapa kuna mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia biashara ya nguo.
- Kununua nguo na kuuza kwa reja reja.
-
Kununua nguo na kuuza kwa jumla.
-
Kuagiza mzigo kutoka viwandani au nje ya nchi na kuuza kwa jumla au reja reja.
-
Kuwa na kiwanda kinachotengeneza mavazi.
-
Kuwa mbunifu wa mitindo mbalimbali ya mavazi.
-
Kuandaa maonesho ya mitindo ya mavazi.
-
Kushiriki maonesho mbalimbali ya mavazi.
-
Kufanya masoko kwa wenye biashara ya mavazi na ukalipwa kwa kamisheni kwa mauzo yanayotokana na masoko yako.
-
Kutumia mitandao ya kijamii kutangaza mavazi na kuuza hata kwa walio mbali.
-
Kukodisha mavazi ya matukio maalumu kama sherehe na mengineyo.
Unapokuwa ndani ya biashara hii na hata nyingine yoyote, orodhesha njia zote unazotumia kuingiza kipato na jiulize njia zipi zaidi unazoweza kutumia.
Hapo utaweza kuziona fursa nyingi.
Kocha.