
Watu huwa siyo wepesi kusema hapana, wanajua wakikuambia hapana watakuumiza. Hivyo wanatafuta kauli ya kukuambia hapana bila kukuumiza.
Na kauli rahisi huwa wanakuambia watakutafuta wakiwa tayari. Ukikubaliana na kauli hiyo na kusubiri wakutafute, utasubiri sana na hawatakutafuta.
Badala ya kukubaliana nao tu kirahisi, waombe wakuambie lini watakuwa tayari, wakupe tarehe kabisa. Na pia endelea kuwasiliana nao mara kwa mara ili wasikusahau kabisa.
Kwa kila fursa unayopata ya kuwasikiana nao itumie. Hilo litakuweka kwenye fikra zao na watashawishika kufanya kile unachowataka wafanye.
Ukurasa wa kusoma ni kujiweka kwenye fikra zao; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/06/14/2357
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma