Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia ufundi wa simu.

Karibu kila mtu sasa anatumia simu ya mkononi.
Kwa mazingira ya wengi, simu zao zimekuwa zinaharibika mara kwa mara na kuhitaji matengenezo.
Hilo linatoa fursa mbalimbali za kuingiza kipato kupitia ufundi wa simu.

Hapa kuna mawazo kumi ya kuingiza kipato kupitia ufundi wa simu.

  1. Kuwa fundi unayetengeneza simu.

  2. Kuuza vifaa mbalimbali vya simu.

  3. Kununua simu zilizoharibika, kuzitengeneza na kuziuza.

  4. Kuuza vifaa vya kutengeneza simu kwa mafundi wengine.

  5. Kuwa na mashine za kutengeneza simu na kutoa huduma kwa mafundi wengine.

  6. Kuwafundisha wengine kutengeneza simu.

  7. Kuandaa mafunzo ya utengenezaji simu na kuweka kwenye mtandao kama youtube na kupata fedha kwa matangazo.

  8. Kuuza simu.

  9. Kuagiza simu na vifaa vyake kutoka nje ya nchi na kupata faida zaidi.

  10. Kuajiri mafundi simu na kutengeneza simu zaidi za wateja hivyo kuingiza kipato zaidi.

Kocha.