Mawazo 10 ya kuingiza fedha kwa shule ya sekondari.

Elimu ni hitaji la msingi kabisa la watu.
Licha ya serikali kutoa elimu bure, bado ubora wa shule za serikali haujawa mzuri, hasa upatikanaji wa walimu na vitendea kazi mbalimbali.

Hii inatoa fursa kwa wanaoweza kutoa elimu bora ya sekondari kuweza kufungua shule zinazotoa kile kinachokosekana kwenye shule za sekondari.

Hapa kuna mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia shule ya sekondari.

  1. Kuandikisha na kufundisha vizuri wanafunzi na kulipwa ada.

  2. Kuwa kituo cha kutoa mafunzo kwa wanaorudia mitihani na wakalipia.

  3. Kuwa kituo cha kufanyia mitihani kwa watahiniwa binafsi na wakalipia.

  4. Kufundisha masomo ya ziada kwa wanafunzi mbalimbali.

  5. Kuendesha madarasa ya awali kwa kitado cha kwanza (pre form one) na kidato cha tano.

  6. Kuendesha miradi mbalimbali ndani ya shule au karibu na shule kama duka, stationary, mgahawa n.k.

  7. Kuzalisha mahitaji muhimu ndani ya shule ili kupunguza gharama za kununua.

  8. Kuandaa na kuchapa vitabu au vitini vinavyoweza kutumiwa na wanafunzi ndani na nje ya shule.

  9. Kuwa na mfumo wa kuendesha masomo na mazoezi mbalimbali kwa kutumia mtandao, hasa katika zama hizi za mabadiliko makubwa. Pamoja na kuuza vifaa vya kuwawezesha wanafunzi kujifunza mtandaoni.

  10. Kutumia eneo la shule lisilotumika kuwapangishia wanaoweza kutumia. Mfano badala ya kuwa na uzio ambao ni ukuta, unakuwa ni uzio wa fremu za maduka ambapo watu wanapangishiwa.

Pamoja na ushindani mkali ulio kwenye huduma hii ya shule za sekondari, bado zipo fursa ambazo mtu unaweza kuzitumia vizuri na kuingiza kipato kizuri pia.
Hizi ni za kuanzia, unaweza kufikiria njia zaidi unapokuwa kwenye sekta hii.

Kocha.